Thursday 28 September 2017

UJANA NI MTAJI YAWAFIKIA WAKAZI WAKIJIJI CHA KIDOGOZERO, CHALINZE MKOA WA PWANI.

Programu ya UJANA NI MTAJI inayoratibiwa kwa ushirikiano wa mashirika ya FARAJA TRUST FUND pamoja na LIGHTS UP YOUTH FOUNDATION ilipata fursa ya kuwatembelea wanakijiji wa Kidogozero kilichopo Chalinze mkoa wa pwani takribani km 132 kutoka Mkoa wa Morogoro. 
Mwenyekiti wa kijiji cha Kidegozero Bwana Ali O. Mmanga (katikati) akiwa pamoja na wawakilishi wa programu ya Ujana ni Mtaji.
Safari hiyo iliratibiwa na taasisi ya Agro and Youth Development Network (AYODEN TANZANIA) ambapo UJANA NI MTAJI iliwakilishwa na wataalamu kwenye nyanja ya sheria, kilimo, ufugaji, ujasiriamali na masoko.
Wawakilishi wa UJANA NI MTAJI walifikia ofisi ya kijiji cha Kidogozero ambapo walipokelewa na mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ali O. Mmanga. Baada ya kutia saini kwenye kitabu cha wageni, Mwenyekiti aliongoza msafara kuelekea kitongoji cha Migudeni ambapo mkutano wa kijiji ulitarajiwa kufanyika.
Baada ya kusalimiana na wanakijiji, Mwenyekiti wa kitongoji cha Migudeni Bwana Hassan Ally Tika alifungua kikao na kuwakaribisha wote tayari kwa kuanza kwa agenda mbalimbali.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Migudeni, Bwana Hassan Ally Tika akifungua kikao 
Baadhi ya wanakijiji cha Kidegozero wakimsikiliza mwenyekiti wa kitongoji cha Migudeni Bwana Tika wakati wa ufunguzi wa kikao.
Mwenyekiti wa kitongoji migudeni alimkaribishi maratibu wa mkusanyiko huo kutoka shirika la AYODEN TANZANIA ndugu Joseph Rwehumbiza alimkaribisha kiongozi wa msafara kutoka programu ya Ujana ni Mtaji ndugu Fredrick R. Manning ajitambulishe na kutambulisha wataalamu aliokuja nao.
Ndugu Joseph Rwehumbiza kutoka AYODEN TANZANIA ambaye ndiye aliyekua mratibu wa mkutano.
Kiongozi wa msafara kutoka programu ya Ujana ni Mtaji ndugu Manning alijitambulisha na kuzungumzia kuhusu programu kwa ufupi kwa wanakijiji wa Kidogezero na kabla ya kumaliza aliwatambulisha wataalamu aliokuja nao. 
Ujana ni mtaji kupitia kitengo cha msaada wa kisheria iliwakilishwa na mwanasheria ndugu Derick Vicent ambaye alizungumzia masuala mbalimbali ya sheria hasa upande wa namna ya umilikaji wa ardhi kwa maeneo ya vijijini.
Mwanasheria kutoka programu ya Ujana ni Mtaji ndugu Derick Vicent akizungumza na wananchi wa Kidegozero
Baada ya mwanasheria kuongea masuala mbalimbali kuhusiana na ardhi, alifuatia mtaalamu wa kilimo ndugu Saadan Edson ambapo alizungumza mengi kuhusiana na namna ya kulima kilimo bora na chenye tija. Wananchi walifurahi sana na waliuliza maswali mengi ambayo yote yalijibiwa kiufasaha na kitaalamu.
Mtaalamu wa kilimo kutoka programu ya Ujana ni Mtaji ndugu Saadan Edson akitoa maelezo juu ya njia bora za kufanya kilimo chenye tija.
Baada ya wananchi wa kidegozero kupewa elimu ya kilimo ikiwemo kilimo cha mbogamboga , alifuata ndugu riziki ambaye ni dokta wa mifugo.
Ndugu Riziki kutoka programu ya Ujana ni Mtaji ambaye ni Daktari wa mifugo akiwaelezea na kujibu maswali ya wananchi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na mifugo.
Baada ya mafunzo mafupi upande wa sheria, kilimo na ufugaji ilifuata kitengo cha ujasiriamali na masoko ambapo ndugu Fredrick Roy Manning alitoa alimu kwa ufupi na kujibu maswali mbalimbali yaliyotoka kwa wananchi wa kijiji cha Kidegozero.



SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: